Safari ya Kurudi nyumbani kwa baiskeli

Chile to kili, ni safari ya baiskeli kuanzia Amerika kusini kurudi nymbani Kilimanjaro, Tanzania. Mwezi wa kwanza 2012 niliondoka nyumbani Arusha kuelekea Argentina  ambako nilianja safari ndefu ya kurudi nymbani kwa baiskeli. Naamini kwa watu wengi watafikiri huu ni upungufu wa akili, nakubaliana nao kwasababu hata mimi kwa mara ya kwanza nilipofikiri kuendesha baiskeli kuanzia Arusha mpaka Marangu, nilijiambia haiwezekani lakini ni kwa msukumo wa kipekeena imani tu unaweza kufanya vitu visivyo wezekana kuwezekana.  Ndio, nilenda marangu kwa bibi yangu aliyenikuza kwa baiskeli, anafahamu tabia yangu vizuri lakini sasa aliona ninavuka mipika! Baadae nilenda Dar es saalam na rafinki yangu Jacob na baada nilisafiri nchi 16 za Afrika kwa usafiri huo hou. Usifikri mimi ni mwana mashindano, la hasha, ‘kikorokoro’ baiskeli ya mbao unayo sukuma juu ya mlima alafu unaendanayou bondeni ndio baiskeli yangu ya kwanza. Nikuwa na miaka takribani 17 ndio nilijifunza kuendesha baiskeli ya ukweli. Baiskeli kwangu ni chombo rahisi gara nafuu na rafiki wa mazingira, ninatumia chombo hichi kwa uhamasishaji  wa uhifadhi wa mali asili na mazingira na unaweza kufanya lisili wezekana kuwezekana si baiskeli pekee!

Chile to kili ni mradi ambao unamalengo matatu makubwa; Kuhamasisha uhifadhi wa maliasili na mazingira, kuchangisha ada kwa wanafunzi wa kitanzania kuweza kupata nishani yakwanza ya ekologia na wanyama pori (nikiwa ni mmoja wa wanafunzi hao) na pia ni kusisimua vijana kufanya mambo yantakayo wajenga wao na jamii kwa ujumla, labda si kusafiri na baiskeli eeh!

Mradi huu ninautekeleza kupitia shirika lisilo kuwa la kiserikali ambalo nimekuwa mfanya kazi wa kujitolia kwa miaka 3 sasa, Conservation Resource Centre

Kama nivyo sema hapo juu, it kuwa ni upungufu wa akili mtu kuendesha baiskeli kilomita 100, watanzania wengi au wafrika kwa ujumla swali lao kubwa ni; Shilingi ngapi utapata ukimaliza? Wengine huwa wananiambia ‘Utakuwa tajiri sana ukimaliza!’ Nafikiri kama unataka kuwa tajiri unaenda mererani au mwadui! Na kama nikushinda pesa unafanya mashindano!

Kwangu ni tofauti ni imani iliyo jengwa na changamoto nilizopitia, changamoto hizi zimerebwa na uzuri wa uasili. Hii ni kuanzia nikiwa mto mdogo, nimukilia kijijini, motto wa bibi, uchumi ni kuuza ndizi tunune samakina na mafuta ya taa, kaptula ya shule ni suruali ya mjonba.Tofauti na motto wa bibi watoto wengine walikuwa na nafarisi ya kupata vitu vya kuwafurahisha kwa muda, viatu vipya, nguo, nk. Daraja ndogo lilojegwa lili nipatia wakati wa kutumia muda mwingi kugundua vitu ambavyo vilionekana nivya kawaida sana na hivukuwa na umuhimu. Nilianzisha urafiki mkubwa na ndege, panzi, popo, mimea mbali mbali, nk.  Nilianza kuvutiwa na uzuri na tabia za hivi vitu hii ilipelekea kutaka kujua zaidi na zaidi, nilikuta nikitumia muda mwingi msituni, mtoni, kwenye miti, nk. Baadae nilikuja kujifunza uhisiano wa kila kitu knacho tuzungnga sisi binadamutukiwa nisehemu ya huu mfumo lakini tratibu tulianza kujitoa na sasa imepelekea uharibifu mkubwa, dunia ambayo mababu zetu waliishi haitakaa iwe ile ile kamwe; Ongezeko la joto dunia ni janga kubwa kuliko tunavyo weza kufikiri.

Sasa anamini unaweza kuona kwamba ni vitu gani vinavyo weza kukufanya uendeshe baiskeli kwa kilometa100-150, kupanda milima kama Andes, kwenye baridi ya Amerika kusini, kwnye joto na ukame kama jagwa la Atacama, kupita kwenye tmadunini mbali mbali, kujifunza utu na ukarimu pale mtu anaposimama na kukupatia maji ya kunya au sehemu ya kula, kunyanyapaliwa, nk.

Ninafanya midahalo na mazungumzo na wanafunzi, jamii kwa ujumla kupitia vyombo vya habari, kwa kusafiri kwa baiskeli nina tumia nafasii hii kuhimiza uhifadi wa mali asili na mazingira kwa maendeleo endelevu. Naamini katika elimu, tukipata elimu sahihi tunaweza kufanya ulimwengu ukawa sehemu salama na  nzuri kwa kila mmoja. Msukumo mkubwa wa mradii huu ni kutokana na changamoto nilizopitia mimim mwenyewe na vitu nilivyo jifunza. Si hitaji kuzungumza kwa undani juu ya elimu Tanzania au Afrika kwa ujumla, ni hali iliyo wazi kwa kila mmoja. Niljaribu kuchukua hali yangu na kufananisha na vijana nilikutana nao wakati ninasafiri Tanzania na nje ya Tanzania. Baada ya jitihada za muda mrefu sasa ningeweza kupata elimu ya juu na kutoa mchango mkubwa lakini hali niliojione ilinifanya nifiri zaidi. Kwa mara nyingine nitatumia hii baiskeli kuhimiza watu kuchangia fedha kwa ajili ya elimu.

Sijawahi kukubalia na neon ‘umaskini’ kwa maranyine kwa watu wengi ninaonekana kama kichaa, hiyo haijalishi kupitia vitabu nijifunza mambo mengi juu ya Tanzania na Afrika. Lakini hii haikutosha pale nilipokuta vitabu vingi vimeandikwa na wageni, sasa ninahitaji kujione na kujifunza mwenyewe. Kwa ujasiri nilijifunza tokiea nikiwa mototo niliamua kutumia baiskeli kusafiri kujione hali halisi ya Nchi yangu na bara langu.  Baada yah ii safari nilijikuta nikiwa na nguvu zaidi, ufahamu nilioupata uliongeza simenti katika ile emani na uelewa niliokuwa nao, sasa ninaweza kusimama na kusema yale ninayo amini. Utumwa, ukoloni na ukoloni mambleo uliliacha bara katika giza nene lakini historia hii yote imejenga watu wasio na mfano. Mfano huu tunaweza kuutumia kuendele kujijenga na kujenga jamii kwa ujumla.

Miezi 7sasa,nchi 6,kilometa 8000, nina zidi kujione changamoto za kimazingira kadri baiskeli invoyo nipeleka kasikazini, kujifunza tamaduni mbali mbali na kujionea majabu ya dunia.

Amerika kusini Argentina, Chile, Peru, Bolivia nchi ambazo zinategemea maji kuttoka milima ya Andes zinazidi kuwakame kadri barafu invyo yeyukasiku hadi siku. Brazili, Nchi amabayo inasehemu kubwa yam situ wa Amazoni, msitu amabo unategemewa na dunia nzima kwa ajili ya kusafisha kaboni monoksidi. Kuanzia mwaka 1990 ilianza kubadilisha sera zake kuhusiana na matunizi ya msitu kwa maendeleo yake kuongeza mashamba makubwa kwa ajili ya uzalishaji rahisi. Manedeleo ya siyo endelevu yamepelekea kujenga mamia ya mabwa kwaajili ya uzalishaji wa umeme. Hali hii imepelekea mabadiliko ya shemu kubwa yam situ kuwa nyika. Nyika nyingine tayari zimeanza kuwa kame na nyingine ziko hatarini kwa moto.

Hii ni baadhii tuya mifano ya maendeleo ambayo yanachangia mabadiliko ya tabianchi na ongezeko la joto, sisi tukiwa kwa nchi za ulimbwengu wa tatu tupohatarini zaidi, kwa ukamame, mafuriko, nk. Nchi tajiri na kubwa kiviwanda zipo katika msukumo wa kubadilisha mfumo lakini kutokana na siasa, kuzoea mfumo Fulani na upinzania kati ya nchi tajiri nazinazo kuwa Marekani, Nchi za ulaya, China, Brazili, n.k hakuna suluhisho la karibuni. Sasa tuna 390 ppm (part per millon) kaboni dioksidi angani ambayo inazalishawa na uchomaji wa mafuta (magari), viwanda, matumizi ya makaa yamawe, n.k Asilimia 92 ya watu wazima marekani wanamiliki gari! Hali hii inanifanya niji ulize; Je sisi mchi zinazo endelea tunataka kuendelea katika mfumo huu?

Uhuru na tamaduni…

Katika mambo niliyo jifunza ni nchi kama Tanzania tunamefikia uelewa wa hali ya juu labda bila hata kujua.Kwetu sera za uhamiaji na uhuru wa binadamu pamoja na ukarimu  kwa kiasi Fulani zipo katika kiwango cha juu. Changamoto kubwa ninayo kutana nayo ni kupata vibali, visa. Nchi nyingine zimekataa kunipatia visa bila sababu wakati vigezo kwa nchi nyingi vikionyesha wazi kwanba vinakuzuia, hii inaweza kutasfsiriwa kama ubaguzi. Nakama tuna vyo fahamu ubaguzi ni ujinga wa hali ya juu, kutoweza kufahamu kwamba binadamu wote ni sawa na kuendeleza ubaguzi ni kusababisha matatiozo ya kisaikolojia kwa muathirika!. Nchi pekee amabayo suku hitaji visa na niyou karibishwa na kujisikia huru ni Bolivia.

Sisi Waafrika ldba ni watu wa kipee sana, kwa rangi, historian a kila kitu. Katika nchi za Argentina, Chile, Bolivia hata Meksiko kuona mtu mweusi ni kama bahati. Bolivia walikuwa wanashangaa kama hii ndio rangi yangu na je huwa nanyoa nywele kila wiki? Wnawake na watoto vijini walikuwa wanakimbia wakiniona, hotelina na dukani wakati mwingine ilikuwa ni shida kupata huduma. Ninapozunguza kispaniola mara ya kwanza hawaamini kwa nina weza kuzungumza luga yao.  Kwenye miji mikubwa watu wengi wanaomba kupiga picha.

Kama Afrika tunavyo ita wazungu Amerika kusini pia wananita ‘Negro’ Cheusi lakini kwa nchi kama Brazili, Colombia, Marekani watu wana ogopa kutamka nene lolote litakalo ashiria ubaguzi wa rangi sana, sana kwa watu weusi.

Tamaduni ni vitu ambavyo vinasisimua, Amerika Kusini tamaduni utamaduni wake unaonekana kwenye Ukristo wa katoliki, mziki, vyakula; utamaduni huu una uhusiano mkuwa na walationo ambao ni sehemu kubwa. Wahindi wa Amerika watu wakwanza kuishi katika haya mabari wengi wao wali uwawa na watawala  wa kispaniola, utamaduni wao hauna tofauti sana na wakiafrika, wana miungu mbalimbali, n.k Kwa sasa ninajifunza utamaduni ambao umeenea sehemu kubwa duniani kupitia mziki, filamu, n.k; Utamaduni wa wamarikani, Je huu utamduni wa uhuru wa hisia, mavazi, n.k umetoka wapi?

Nimejaribu kuandika kwa kifupi lakini siwezi kuandika kila kitu hapa lakiniunaweza kufikii uzoefu wa kuw nje ya bara kwa mara ya kwanza, kusafiri kwa baiskeli an tabia ya kupenda kujifunza kila kitu, ni uzoefu ambao unaweza kujaza kitabu eeh! Ni nabaki katika malengo ‘Uhufandhi wa mali asili na mazingira kwa maendeleo endelevu na elimu’

Mpaka sasa sija sehemu kama Afrika au nchi kama Tanzania, tumejaliwa utajiri mkubwa wa maliasili isiyo patikana shemu yoyote,  tamaduni mbalimbali, ufahamu na uelewa unaotuwezesha kuishi pamoja achilia mbali tofauti zetu, n.k. Tunahitaji kuvifahamu zaidi, kuhifadhi na kutunza vitu hivi. 

This entry was posted in Uncategorized. Bookmark the permalink. Follow any comments here with the RSS feed for this post. Post a comment or leave a trackback: Trackback URL.

4 Comments

 1. Posted September 7, 2012 at 7:24 pm by Meshack Sospeter | Permalink

  Elvis Munis ninafatilia safari yako tunajifunza mengi ya wenzetu kutokana na unayopitia ni safari inayohitaji uvumilivu mkubwa toka siku tulipoelekea Dar mpaka Leo bado unaendesha!! Lini utamaliza? Inahitaji moyo wewe ni kioo cha jamii uskate tamaa .mi nashangaa kama sisi kuingia nchi zao inakuwa shida kwa nini wao kwetu wanaruhusiwa kuingia?

  • Posted September 8, 2012 at 4:54 pm by Elvis | Permalink

   Meshack! Habari za siku bwana? Siku nyingi sana, nashukuru bado unafuata safari yangu. Ka nchi nyingi za africa kuanzia siku miaka hiyo 1400 mpaka leo ni mppango ule ule. Kutokana na historia na hali ya kiuchumi kupata visa ukiwa na pasi poti ya nchi za Africa inakuwa ngumu. Lakini sisi tumezoea changa moto bwana.

 2. Posted September 8, 2012 at 11:07 am by Tanisha | Permalink

  I truly love your website.. Pleasant colors & theme. Did you make this
  website yourself? Please reply back as I’m hoping to create my very own blog and want to find out where you got this from or just what the theme is called. Thanks!

  • Posted September 8, 2012 at 4:58 pm by Elvis | Permalink

   Tanisha, The web is created by my friend Ryan (chaos designorder), he will be happy to assist you with your requirements Ryan Paetzold (ryan@chaosdesignorder.com)

Post a Comment

Your email is never published nor shared. Required fields are marked *

*
*

You may use these HTML tags and attributes: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>